Hamisa Amtupia Diamond Dongo Kuhusu Uchawi

Ni siku kadhaa zimepita tangu Hamisa alipatwa na skendo ya kumloga Diamond na kuvuja kwa sauti za Hamisa akiongea na waganga ili waweze kumtengeneza Diamond ili aweze kuijali familia yake na kumjengea nyumba.

Diamond alilalamika sana kuhusu swala hilo na baada ya hapo Hamisa alikiri kuwa ni kweli sauti ilikuwa ni ya kwake lakini hakuwa anamloga bali alikuwa anaongea na shekhe na kumuelezea matatizo ya mahusiano yake ili aweze kufanyiwa dua.

katika pitapita na kukutana na comments moja ya hamisa akimjibu shabiki yake kuhusu  maswala ya uganga na uchawi ambapo  kwa jinsi hamisa alivyojibu inaonekana kuwa dongo hilo lilikuwa linamlenga mzazi mwenzie huuyo kwa sababu Diamond ndio aliekuwa akilalamika baada ya kusikia kuwa Hamisa alikuwa akitaka kumloga, katika comments hizo,mambo yalikuwa hivi  ;-

‘MWANAUME KULIA MITANDAONI ETI UNALOGWA HUO NI  UMAMA, MWANAUME UNATAKIWA USEME BEIBY ONGEZA KUNILOGA NIKUONGE DUNIA” ambapo hiyo ilikuwa ni maoni ya shabiki na Hamisa alijibu  “TENA KUSEMA ONGEZA KUNILOGA NI UMAMA UNATAKIWA UWE MGANGA ILI KWENDA SAMBAMBA.