Hanspope Afikishwa Mahakamani Kusomewa Mashtaka Yanayomkabiri

Mwenyekiti wa Simba, Zacharia Hans Poppe ameachiwa kwa dhamana baada ya kusomewa mashitaka mawili katika mahamaka ya Kisutu jijini Dar es Salaam.

Kutoa taarifa ya uongo kwa TRA kuhusiana na nyasi bandia, kwamba alitaja bei kubwa zaidi, Shitaka la pili, nyaraka za nyasi bandia hazikuwa za ukweli, anatuhumiwa kuzigushi.

Dhamana yake ina thamani ya Sh milioni 30 kwa watu wawili, kila akiweka ya Sh milioni 15, Kesi hiyo imeahirishwa hadi Ijumaa Oktoba 19 itasikilizwa.

Hans Poppe amerejea nchini na kujisalimisha kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Hans Poppe ameunganishwa kwenye kesi ya kugushi nyaraka na utakatishaji inayowakabiri Rais wa Simba, Evans Aveva na makamu wake, Geofrey Nyange ‘Kaburu’.