Mchekeshaji Idris Sultan ametumia ukurasa wake wa instagram kuwauliza mashabiki zake ni nani yupo tayari kula hela zake za Bongo Star Search(BSS) endapo ataibuka mshindi wa mashindano hayo.

Kutokana na kile ambacho amekiandika Idris Sultan kwenye ukurasa wake wa instagram comments zimekuwa nyingi kwenye post hiyo, Wema Sepetu akiwa miongoni mwa watu waliocomment na kusema kuwa anaambiwa apewe yeye kutokana na wengi kumshutumu kuwa alikula hela za Big Brother Africa.

Idris Sultan alicomment kwa utani kwa kumjibu Wema Sepetu  na kusema “Kuna siku niliweka dola mbili kwenye meza nikakuta unaila bisha” iliwahi pia kusemekana kuwa Wema Sepetu ndio aliyemaliza hela za Idris Sultan kipindi aliposhinda Big Brother 2014.