Irene Uwoya amruhusu Dogo Janja kuoa mke wa Pili

Msanii wa filamu, Irene Uwoya amesema hana shida iwapo mume wake, Dogo Janja ataamua kuoa mke wa pili.

Utakumbuka May mwaka huu muigizaji huyo alikaririwa akisema kuwa hayupo tayari kwa Dogo Janja kuoa mke wa pili ila kwa sasa amesema kwa sababu dini ya mume wake inampa ruhusa hana shida na hilo.

“Hapana hayo ni maamuzi yake, kwani ni kitu kibaya, yeye si ni muislamu?, sianaruhusiwa kuoa wake wanne, ?, of course why not,” Irene Uwoya ameiambia The Playlist ya Times FM.

Dogo Janja na Irene Uwoya waliripotiwa kufunga ndoa November 25, 2017, hata hivyo ni vigumu kutaja tarehe kamili kutokana na namna walivyoliweka suala hilo hasa kwa upande wa vyombo vya habari na mitandao.