Kidoa Ajisifu Kukulia Uswahilini " Tuliokulia Huko ndo Tunaofanikiwa Kimaisha"

MSANII wa fil amu ambaye pia alikuwa muuza sura kwenye video za Kibongo, Asha Salum ‘Kidoa’ amejisifu kukulia uswahilini na kusema kuwa wasichana wengi ambao maisha yao wamekulia huko ndiyo wanaofanikiwa kimaisha.

Kidoa alisema kuwa, mtu aliyekuwa akimuona akiwa katika maisha ya uswahilini hawezi kumtarajia leo anaweza akasimama sehemu yoyote na mtu akamsikiliza na hiyo yote ni kuona kuwa anapoendelea kukua hataki kurudi maisha aliyopitia hivyo kila kukicha ni kutafakari kitu cha kufanya.

“Unajua ukiwaona wasichana wengi wamefanikiwa ambao ni warembo huwezi kuamini kama wametoka uswahilini, tena kwenye maisha ya taabu sana, lakini mwisho wa siku wanakuwa kioo cha jamii, kama leo hii mtu hawezi kujua kama nilitokea uswahilini kwenye kila kituko, lakini angalau naweza kusimama popote na nikasikilizwa ninachokiwakilisha kwa wakati huo,” alisema Kidoa.