Msanii wa Bongo Fleva, Cassim Mganga amesema muziki huo ukiwa na waimbaji wanne kama Mbosso utafika mbali zaidi kutokana na uimbaji wake na ni kitu ambacho alikuwa anakipigani kwa muda mrefu.
Muimbaji huyo akizungumza na Wasafi TV amesema mahadhi ya muziki anaofanya Mbosso kwa sasa amekuwa akiyapigania pekee yake kwa kipindi kirefu sana hivyo anafurahia kuona wasanii wengine wanafuata nyayo zake.

“Ni moja ya matunda ambayo nayafurahia sana, so wakiongezeka kina Mbosso wengine kama wanne itakuwa poa sana na itakuwa heshima kubwa sana kwangu kwa hakuna kitu kizuri kama kufanya jambo baadaye likaja kuwa na matunda, so furahia sana na nina-bless sana na nilishafanya hivyo,” amesema Cassim.

Mbosso kwa sasa anafanya vizuri wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la Hodari. Utakumbuka usiku wa January 27, 2018 ndipo Mbosso alitambulishwa kuwa chini ya lebo ya WCB na kutoa wimbo wake wa kwanza uitwao Watakubali.