Mwanamuziki wa Bongo fleva na Mshehereshaji (MC) maarufu kama Mimi Mars amefunguka na kuweka wazi kuwa hakuna kitu anapenda duniani kama Mapenzi.

Mimi Mars amefunguka hayo Kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi cha Refresh cha Wasafi Tv, ambapo amekiri kuwa yeye ni mtu wa mapenzi sana kiasi ya kwamba hata akikutana na jambo lolote linalohusu mapenzi basi huwa Makini.

Mimi napenda sana mapenzi hata kama kuna story ya mapenzi kuna sehemu imeisha ukianza kuwa na Mahusiano na mtu mwingine unaanza upyaa, ina maana uneshasahau yale ya nyuma kimeanza upya Coz you know mapenzi yanarun dunia”.

Mimi Mars anayetokea Kwenye Familia ya Kimuziki kuanzia dada yake Vanessa Mdee anayefanya muziki wa Bongo fleva mpaka dada yake mwingine ambaye pia ni msanii wa nyimbo za injili, ameendelea kufanya vyema na ngoma yake ya ‘Kodo’.