Odama: Msimamo Wangu Unaniponza Watu Wananiona Ninaringa

STAA wa filamu kutoka Bongo Muvi, Jennifer Kyaka ‘Odama’ amefunguka kuwa siku zote amekuwa mwenye msimamo na kusimamia jambo lake, lakini anapofanya hivyo watu wanamchukulia tofauti na kumuona kama anaringa na asiyependa kusikia mtu na hicho ndicho kinamponza.

Odama aliliambia Ijumaa Wikienda kuwa amejifunza kitu kikubwa kwenye maisha kupitia mama yake mzazi kwamba, kuwa na msimamo ndicho kitu muhimu kwenye maisha na ndicho anachofanya na hadi sasa amefanikiwa katika mambo yake mengi.

“Kikubwa ni kuwa na msimamo katika mambo yako mengi ndiyo unaweza kusonga mbele zaidi na siyo vinginevyo. Ndiyo maana watu wengi wananiona tofauti kama ninaringa na nisiyependa kusikia cha mtu mwingine kumbe ni msimamo wangu tu ndiyo unaniponza nionekane hivyo,” alisema Odama.