Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli, amemteua Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani, Mh. January Henry Msofe kuwa Mwenyekiti wa tume ya kurekebisha sheria.

Mbali na Mwenyekiti huyo mpya wa Tume hiyo, Rais pia amewateua Bw. Iddi Mandi na Bw. Julius Kalolo ambao wanakuwa Makamishna wa muda wa tume hiyo.

Katika hatua nyingine, Rais pia amemteua Bw. Paul Kimiti kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ranchi za Taifa (NARCO).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ikulu,  Uteuzi huo uliotangazwa leo Oktoba 16, 2018 umeanza tangu Oktoba 14, 2018.