Mwanadada Irene Uwoya amefunguka na kusema kuwa katika watu anaotamani sana kufanya nao kazi ya sanaa hasa kuigiza ni msanii wa bongo fleva Juma Nature kwa sababu hata hivyo hajawahi kufanya nae kazi yoyote  tangu ameanza kazi yake ya sana.

Irene ameongea hayo alipokuwa akiongea na Times Fm na kusema kuwa moja ya sifa kubwa ya kutamani kufanya kazi na juma anature ni kwa sababu muoekana wa msanii huyo ni uhusika tosha katika kufanya kazi ya kuigiza .

Kama kuna msanii wa bongo fleva natamani kufanya  nae kazi ( movie) basi ni Juma Nature,  maana jinsi alivyo tu tayari anakuwa ameshava uhusika.

JUma nature alikuwa moja ya wasanii waliwahi kufany avizuri sana hapo miaka ya nyuma na mziki wake kupendwa sana na vijana.