Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (katikati) akizungumza na Watendaji Wakuu wa Wizara na Taasisi zake katika kikao cha kujadili masuala mbalimbali yakiwemo utendaji kazi wenye weledi. Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa ofisi ndogo ya Wizara, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto meza kuu ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali, Jacob Kingu. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Ramadhan Kailima.

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (katikati) akimfafanulia jambo Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, (CGP) Phaustine Kasike (kulia aliyesimama), katika kikao cha kujadili masuala mbalimbali ya utendaji kazi wa Wizara hiyo. Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa ofisi ndogo ya Wizara, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto meza kuu ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali, Jacob Kingu. Kulia meza kuu ni Naibu Katibu Mkuu, Ramadhan Kailima.

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (katikati) akimsikiliza Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara hiyo, Wanja Mtawazo, wakati alipokua anatoa taarifa yake katika kikao cha watendaji wakuu wa Wizara na Taasisi zake kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi ndogo ya Wizara, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto meza kuu ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali, Jacob Kingu. Kulia meza kuu ni Naibu Katibu Mkuu, Ramadhan Kailima.

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (katikati) akimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali, Jacob Kingu (kushoto), alipokua anamfafanulia jambo katika kikao cha watendaji wakuu wa wizara na taasisi zake kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi ndogo ya Wizara, jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Ramadhan Kailima. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.