Msanii wa muziki Bongo, Barakah The Prince ameweka wazi kuwa ameachana na mpenzi wake, Naj.

Muimbaji huyo amesema ilifikia hatua kuwa mapenzi yao hayawezi kuendelea tena hivyo kila mmoja kuendelea na maisha yake ila kuachana kwao sio kwa ubaya.

“Kuna vitu huwa vinatokea hadi kuachana lakini sio kila kitu unaweka wazi, tena vitu person vya kimahusiano nitakuwa namkosea hata heshima yeye mwenyewe na vile vile naamini kila kitu huwa kinapangwa na Mungu,” anasema.

Licha ya kuwa wapenzi Barakah The Prince alikuwa akifanya muziki na Naj kupitia lebo yake ya Ban Music.