Mwanangu ndio sababu ya kuacha kudanga’-Gigy Money

Ikufikie sababu ya msanii Gigy Money kuachana na tabia aliyokuwa nayo miaka kadhaa iliyopita ambapo alikuwa akipatiwaa hela na wanaume waliomzidi umri ‘Sponsors’ ili kukidhi mahitaji yake pamoja na kumsaidia mama yake mzazi.

Kupitia mahojiano aliyoyafanya Gigy Money na kituo cha Televisheni cha BBC katika kipindi cha The she word amefunguka na kusema kuwa ameachana na tabia hiyo kwa sababu mwanae Myra ndio amebadilisha maisha yake na hataki mwanae aishi maisha aliyopitia.

” Nilikuwa nina miaka 17 nilikuwa najua nini nafanya na niliona ugumu aliyokuwa akiupata mama yangu mara nyingi tunafanya ili kupata hela lakini hatupendi hata kama ni njia rahisi ya kupata hela,Kilichonifanya nibadilike ni mwanagu sitaki aje kuwa kama mimi”