Mwanadada Irene  Uwoya hivi karibuni aliropitiwa kuwa amechana na mwanamme aliefunga nae ndoa ili kufunga ndoa na tajiri mwingine kimya kimya, Irene ambae alifunga ndoa mapema mwaka huu inasemekan kuwa ndoa hiyo na msanii dogo janja imeota mbawa na wawili hao kwa sasa hawapo tena pamoja.

Hata hivyo Uwoya aliulizwa kuhusu tetesi za kuolewa na mwanaume mwingine , lakini alikataa na kusema kuwa hakuna kitu kama icho watu wamekuwa wakiongea tu.

Hapana , hakuna kitu kama icho,mimi nilikuwa kwenye sherehe jana,kwanza siwezi kuongelea mambo yangu ya ndani kias icho labda kama kuna mambo mengine.

hata hivyo tetesi za kuolewa tena kwa uwoya zinakuja baada ya mwanadada huyo kuonekana kuwa ameachana na mume wake lakini bado amekuwa akionekana mitandaoni akienda sehemu mbalimbali za gharama na kuvaa nguo za gharama sana kitu mabacho hakikuwepo hapo awali alipokuwa kwenye ndoa.