Mara kadhaa msanii Msami amekuwa akikutana na maswali kizushi kuhusiana na ndoa ya Dogo Janja kutokana aliwahi kuwa na mahusiano na Irene Uwoya.

Sasa kwenye mahaojiano na Wasafi TV aliulizwa ni kitu gani ambacho hapendi kwenye mahusiano  na kueleza kuwa hawezi kushiriki ndoa kwa ajili ya kutengeneza stori.

“Siwezi kushiriki ndoa ambayo inataka kutengeneza trend, inataka tu kutengeneza stori, no!,” amesema Msami.

Tangu Dogo Janja na Irene Uwoya kufunga ndoa amekuwa hawakauki kwenye vyombo vya habari na mitandao na sasa kuna tetesi zinafukuta kuwa ndoa yao imevunjika ingawa wenyewe wamekuwa wakikanusha hilo.