Linah aanika ukweli kuachana na mume wake

Msanii wa muziki wa Bongofleva, Linah Sanga amefunguka juu ya taarifa za kuachana na baba mtoto wake ambaye anatajwa kuwa mume wake, Shaban Mchomvu.

Akizungumza na www.eatv.tv, Linah amesema hajaachana na mume wake huyo, hivyo tetesi za kuachana hazina ukweli wowote na kusisitiza kuwa anasikia yote yanayozungumzwa lakini anakaa kimya kwakuwa yeye na baba wa mtoto wake wana familia.

“havina ukweli wowote watu wanatengeneza tu, ndio maana mimi nimenyamaza kimya na mwenzangu amenyamaza kimya, tukiviongelea inakuwa sio vizuri kwa sababu unajua tuna familia, amesema.

“Watu wengine wanakuwa shocked(kupata mshtuko) kusikia kitu kama hicho, hamna yeyote kati yetu ambaye amezungumza chochote kama tumeachana”, ameongeza Linah.

Hivi karibuni iliibuka minong’ono kuwa msanii huyo anayetamba na wimbo wa ‘Koleza’ kuachana na mzazi mwenzake, Shaban Mchomvu maarufu kama ‘director ghost’.