Official Lynn Afunguka  Kuhusu Bifu Lake  na Hamisa Mobetto

Mrembo huyo kwenye mahojiano na SnS Tanzania amesema kuwa hana bifu na Hamisa kutokana hawajahi kuonana na pia amemjua hivi karibuni hivyo hamna kitu kama hicho.

“No sijawahi kugombana naye, sijawahi hata kukutana naye, hatujawahi hata kuongea. Unakuwa na ugomvi na mtu wakati hata hatujawahi kuonana,” amesema.

Kwa sasa Lynn anafanya vizuri mara baada ya kutokea kwenye video ya wimbo wa Mbosso, Hodari. Mrembo huyo alipata umaarufu mkubwa alipotoa kwenye video ya Rayvanny inayokwenda kwa jina la Kwetu.