HUSNA AANIKA MAHABA YAKE KWA DIAMOND

MSHIRIKI wa Shindano la Miss Tanzania 2011/12, Husna Maulid hivi karibuni alizua mshangao baada ya kuanika kwamba naye ni miongoni mwa warembo ambao wanatoka kimapenzi na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.

Husna aliweka picha yake kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram na kusindikiza na maneno ‘roho ya simba’ akimaanisha roho ya Diamond na yupo Madale anapoishi msanii huyo hivyo kusababisha watu kumshambulia kwa matusi wakimuuliza inakuwaje anaingia kwa mwanaume ambaye anajua ana wanawake wengine wakati wanaume wapo wengi.

Baada ya kushambuliwa huko, Za Motomoto News ilimtafuta Husna na kumuuliza kulikoni kuingilia penzi la Lynn ambaye anatajwa kuwa ndiye mpenzi wa Diamond kwa sasa ambapo alisema hamuogopi yeyote na kila mbuzi anakula kwa urefu wa kamba yake. “Unajua kila mbuzi hula kwa urefu wa kamba yake, huyo Lynn ni nani, siwezi kumuhofia yeye wala mwanamke mwingine yeyote maana kila mtu na bahati yake, wanaotukana watukane watachoka,” alisema Husna.