Socialite na Video vixen maarufu Kwenye mitandao ya kijamii Irene Godfrey maarufu kama Lynn au Officiallyn ameibuka na kudai hajawahi kuwa kwenye  uhusiano wa Kimapenzi na Diamond.

Lynn alijipatia umaarufu baada ya kutokea kwenye video ya wimbo wa Rayvanny ‘Kwetu’ lakini baada ya hapo amekuwa maarufu kwa kusemekana kuwa Kwenye Mahusiano na Staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz.

Wiki chache zilizopita Lynn alitrend Kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuonekana mikononi mwa Diamond kama mpenzi wake kwa siku kadhaa na hata kudaiwa kumfanyia bonge la Birthday party na hata kumnunulia gari.

Lakini Penzi hilo halikuwa la muda mrefu kwani siku mbili baadae Diamond alionekana na warembo wengine wawili tofauti ikiwemo Tunda na Kimnana ambaye yupo naye mpaka leo.

Sasa Lynn anaibuka na kusema hajawahi kuwa Kwenye Mahusiano na Diamond na kudai ana mpenzi wake ambaye jana tu ametoka kumzawadia gari aina ya BMW.

Kwenye Interview yake na kituo kimoja cha habari Lynn amemwaga povu hili kuhusu Diamond:

Hakuna kitu sipendi kama watu wanao judge watu Kwenye social media na kuongea vitu ambavyo hawavijui kama wewe apo unaponiambia natoka na Diamond! Jamani mimi sipo na huyo mtu nina boyfriend wangu ambaye Yupo Kwenye relationship strong kabisa na muda wowote watu wanaweza kumjua”.

Siju za hivi karibuni Lynn alionekana katika vita ya maneno na wanawake kadhaa wa Diamond kama vile Hamisa, Kimnana na Tunda lakini bado anadai hamjui Diamond na hajawahi kuwa naye.

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.