Msanii wa Filamu Bongo, Rammy Galis amesema kuwa hana mpango wa kuwa kwenye mahusiano msanii wa Bongo Movie.

Muigizaji huyo amesema badala yake labda anaweza kuwa kwenye mahusiano na mrembo kutoka kwenye Bongo Fleva ambaye ni Mimi Mars ingawa hajawahi kukutana naye au kuzungumza.

“May be Mimi Mars, unajua kila binadamu anaumbiwa hisia za kumuona yule ambaye ni tofauti na mwenzako ambaye hajavutiwa lakini

wewe amekuvutia zaidi, hivyo labda ananivutia zaidi,” Rammy Galis ameiambia Cheni TV.

Utakumbuka Rammy Galis alikuwa kwenye mahusiono na muingizaji mwenzie, Agnes Masogange ambaye alifariki April mwaka huu.

Hata hivyo mara kadhaa Mimi Mars amekuwa akikaririwa akisema kuwa hana mpango wa kuwa kwenye mahusiano na mtu yeyote kutoa

tasnia ya burudani Bongo kwa sababu anaona hawataendana, anahitaji mtu wa tofauti kidogo.