Daimond Aomba Ruhusa ya Kuwasha Wasafi Fm

Msanii mkubwa Tanzania na nje ya nchi Diamond Platinumz anazidi kuoyesha juhudi zake katika kufanya muziki wa Tanzania kukua baada ya kuwaomba mashabiki zake kumruhusu kuwasha mtambo wa Wasafi radio kama ilivyokuwa hapo awali kwa Wasafi tv.

Lebel hiyo ya wasafi imekuwa ikifanya vizuri na hata kufanikiwa kufungua tv yao wenyewe na sasa lebel hiyo inataka kufanya kitu kingine kikubwa cha kuwasha Wasafi radio kwa ajili ya mashabiki wao na kukuza muziki na kiwanda cha burudani pia.

Katika ukurasa wake wa twitter, Diamond aliandika ‘naombeni ruksa niwashe @wasafifm”

Lengo kubwa la wasafi ni kutaka kupunguza wimbi la vijana wanaolalamika kila siku kuwa wamekuwa wakibaniwa katika media kuchezwa kwa ngoma zao kutokana na kutokuwa na majina au kusema kuwa hawana vipaji vya kuimba.

Hata hivyo Diamond Platinumza amekuwa mtu wa furaha kufungua media hizi kwa sababu anaamini kuwa zimekuwa zikitatua pia changamoto za ajira kwa baadhi ya vijana katika jamii hasa ple anapowapatia ajira kupitua media zake.

Pamoja na kwamba Wasaf tv haijaanza kurusha matangazo ya moja kwa moja lakini tangu uwepo wke imekuwa ikiwapa nafasi wasanii wengi kuonekana kwa nyimbo zao katika Tv hiyo na kuwafanya kujulikana na kutengeneza mashabiki pia.

Diamond ndio msanii wa kwanza nchini kufungua Radio naTv yake ikiwa ni mojaya ndoto ya wasanii wengi Tanzania