Aikah Afunguka Kuhamia WCB

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Kutoka katika kundi la Navy Kenzo Aikah Marealle amefunguka na kuongolea taarifa za kuhamia WCB.

Baada ya kutoa hit single ambayo inaendelea kufanya vyema mpaka sasa ‘Katika’ waliomshirikisha Staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz kuliibuka tetesi kuwa Nahreel na Aika wamehamia chini ya WCB.

Kwenye mahojiano yake na Global Publishers , Aika  amesema kuwa, amekuwa akisikia kwa watu wengi juu ya kuhamia WCB mara baada ya kuachia wimbo wao  na Diamond jambo ambalo halina ukweli.

Yaani watu wengi wanasema nimehamia WCB lakini ukweli ni kwamba tuna meneja anayetokea huko anaitwa Sallam na amekuwa akitusimamia sasa sijui hayo mengine yanatokea wapi.

Nilikaa na mwenzangu tukatunga Wimbo wa Katika tukaona ni vizuri tukamshirikisha Diamond ndiyo ikawa hivyo sasa nashangaa hao wanaoungaunga maneno”.

Tetesi hizo za Kuhamia WCB zilipamba moto mara baada ya Msanii kutoka WCB Harmonize kusema wazi kuwa wasanii hao wanahamia Kwenye Label yao taarifa ambazo Navykenzo walidai ulikuwa ni utani.