Chuchu Hansi: Mimi na Ray Tayari Mume na Mke Ila Watu Wakae Tayari  kwa Sherehe Yetu

MUIGIZAJI wa kitambo kwenye sanaa ya uigizaji Chuchu Hansi, amefunguka kuwa yeye na mzazi mwenzake Vincent Kigosi ‘Ray’ bado tu kufanya sherehe watu wale wanywe lakini wao tayari ni kama mke na mume hivyo watu wajiandae kwa hilo.

Chuchu alisema kuwa japokuwa wao na Ray wamezaa lakini wamekuwa ni kama marafiki sana na watu wanaoelewana hivyo imebaki tu sherehe.

“Unajua mimi na Ray hatujaamua kuweka wazi tu au tufanye sherehe kwa sababu tumekaa pamoja muda mrefu sana yaani kisheria ni mke na mume hapa kwa mujibu wa sheria, siwezi kusema sherehe ni lini lakini wasubiri,” alisema Chuchu.