Mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema ameendelea na ziara yake ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi katika Kata ya Mchikichini jijini Dar es salaam ambapo kuwanasa vijana 16 wanasadikiwa  kuwa ni wahamiaji haramu.

Naibu Kamishna uhamiaji, Afisa uhamiaji Ilala Pili Zuberi Mdanku kwa kushirikiana na OCD Ilala SP Jason Ibrahim, wamefanikiwa kuwakamata watu hao wanaodaiwa kuwa ni wahamiaji haramu ambapo wamechukuliwa kwa ajili ya mahjiano ili kubaini Kama kweli ni wahamiaji haramu.

Vijana hao wamekamatwa  mara baada ya mmoja wa wananchi kutoka katika kata hiyo kuwasilisha  kero kwa Mjema kuwa kuna nyumba ambayo inawahifadhi wahamiaji haramu, ikiwa Ni mwendelezo was Ziara ya Mkuu huyo.

DCI Pili ameamua kufanya doria katika eneo hilo mara baada ya kupata taarifa hizo kwani, si mara ya kwanza kufanya doria katika eneo hilo na kuwakamata  watu hao wanaodaiwa kuwa Ni wahamiaji haramu.

Amesema kuwa, katika mahojiano ya awali walioyafanya na wahamiaji hao, wamedai kuwa 15 ni watu wa asili ya kigoma na mmoja ni msambaa,  ambapo wamechukuliwa kwa ajili ya mahojiano zaidi.

Kwa upande wake, DC Mjema amewapongeza Afisa uhamiaji Ilala na timu nzima ya OCD kwa kufanya kazi kubwa ya kuwafichua watu hao wanadhani wa kuwa ni wahamiaji haramu.

Amesema kuwa, nchi ya Tanzania haimkatazi mtu kuishi nchini humo, bali itamtaka kila mtu kufata sheria,taratibu  na kanuni za kuishi nchini humo.