Mchekeshaji maarufu Bongo, Lucas Mhavile maarufu kama Joti ameelezea sababu ya kipindi cha vichekesho ambacho walikuwa wanakifanya kila siku ya jumapili wakiungana Wasanii sita kukaa kimya.

Joti amefunguka wakati akipiga stori na Bongo five wakati wa uzinduzi wa vichekesho ambavyo vimerejea kwa sasa ikiwa ni msimu wa pili vinavyojulikana kwa jina la Mwantumu.

Joti amefunguka na kusema “Comedy Show itarejea muda sio mrefu watu watarajie kuwaona Masanja,Joti,Mpoki Wakuvanga,Makregani na Vengu wakifanya kazi pamoja tena”

Joti amefnguka baada ya kuulizwa kwamba kwanini vichekesho hivyo ambavyo walikuwa wakivifanya kila siku ya jumapili wakiungana wasanii sita ambao ni Joti,Msanja,Mpoki,Vengu,Wakuvanga na Makregani,ambao kwa sasa kila mmoja anafanya kazi yeye kama yeye.