Nguli wa habari nchini na Mtangazaji wa Kituo cha Radio cha Kimataifa cha Idhaa ya Kiswahili ya Ujerumani DW, Isaac Gamba amefariki dunia akiwa nyumbani kwake nchini humo.

Inadaiwa Gamba amekutwa akiwa amefariki baada ya Polisi kuvunja mlango wa nyumba yake kufuatia kutoonekana kazini kwake ndipo uongozi wa DW ulipotoa taarifa kwa maafisa usalama ambao walifika nyumbani kwake na kumkuta akiwa tayari ameshapatwa na umauti.

Gamba alipata umaarufu zaidi alipokua akitangaza habari za michezo akiwa na vituo vya ITV na Radio One ambapo alikua akitangaza kipindi cha Spoti Leo kabla ya kuchukuliwa na DW ambapo amefanya kazi hadi umauti ulipomkuta.