Msanii Rich Mavoko amefunguka kuwa amekaa kipindi cha miezi zaidi ya nane bila kufanya show.

amesema kutokana na kukaa muda mrefu bila show atafanya vizuri kwenye jukwaa na Fiesta kwa show zinazofuata.

“Ni muda mrefu sijafanya shoo tangu mwezi wa pili, mwaka huu 2018, naelewa nini nilichokikosa na nitakachokwenda kukifanya kwa mashabiki wangu, wategemee shoo nzuri yenye hadhi na waburudike sio kwenda kutembea tu mkoani’’ amesema Rich Mavoko.

Utakumbuka mwaka 2016 ndipo Rich Mavoko alijiunga na label ya WCB, wimbo wake wa kwanza kutoa chini ya label hiyo unakwenda kwa jina la Ibaki Stori, kisha Kokoro na nyinginezo, pia ameweza kufanya kazi na wasanii wengine nje ya WCB kama Fid Q, Stereo, Nay wa Mitego, Lulu Diva na wengine.