STAA wa Bongo Movie, Jackline Wolper, amesema moja ya ndoto zake kubwa ni pamoja na kuja kuwa mpambaji wa kimataifa ikiwemo Ikulu.

Wolper alisema watu watambue kuwa ana kipaji kikubwa cha kupamba na alianza nacho kabla ya kuwa mwigizaji  na mjasiriamali.

“Mashabiki zangu wachache wasiojua mimi ni mpambaji wa shughuli mbalimbali, nilianza zamani na watu walikuwa wakikubali kazi zangu, ninachoomba kwa Mungu ni uzima na afya kwakuwa nimepanga kutafuta kazi hadi Ikulu,” alisema Wolper.