Mwanadada, Wema Sepetu amemuweka wazi mpenzi wake wa sasa ambaye ameonesha nia ya kufunga naye pingu za maisha siku za hivi karibuni.

Kupitia ukurasa wake wa kijamii wa Instagram Wema amechapisha picha inayomuonesha akiwa na mpenzi huyo kitandani huku akikataa kupokea maoni yoyote kutoka kwa mashabiki wake baada ya kufunga sehemu ya ‘Comment’.

Katika picha hiyo, Wema Sepetu ameambatanisha na maneno,’My future husband’, akimaanisha kuwa huyo ndiye mumewe mtarajiwa.

Muda mrefu Wema Sepetu alikuwa kimya baada ya kumwagana na aliyekuwa mpenzi wake wa muda mrefu, mchekeshaji Idris Sultan.

Mwanadada huyo anatamba na filamu yake mpya ‘Day after death’ aliyoiachia katika siku yake ya kuzaliwa mwishoni mwa mwezi uliopita.