Esha Buheti amwandikia waraka mzito Wema Sepetu baada ya kumtambulisha mumewe mtarajiwa

Kumekuwa na maneno mengi kuhusiana na kile anachokifanya muigizaji Wema Sepetu kwenye ukurasa wake wa instagram baada ya kumpost mpenzi wake mpya na kuandika mume wake mtarajiwa.

Muigizaji Esha Buheti ameonekana kutofurahishwa na kitendo hicho cha Wema Sepetu kuweka mahusiano yake ya kimapenzi kwenye mitandao ya kijamii na kumuambia kuwa mara nyingi huwa anatukanwa kwasababu ya Wema Sepetu na kumuomba atumie kipaji chake vizuri.

“Katika watu walowahi kutukanwa sana sababu yako na mm ni mmoja wapo na najuaa hata leoo hii ntatukanwa sana my dia unapower kubwa sanaa yakufanyaa yalomemaa na watu wakayapokea kwa mikono miwili na sapoti unayo wemaa nimejitahidi kukaa kimyaa nashindwaa na kwasababu nakupendaa sana sanaa sana”

“Ogopa mtu anaekusema mbalii sababu ni mnafki! Wema Mungu alikupa kipaji cha kupendwa sanaa nakuombaa usikitie doa kipaji hicho kuna wakati unakaa kwenye mstarii mashallah nasema yes something big inakuja ilaa ni kama anatokea mtu anaswitch ile line na inakwenda vibaya”

“Wema mamie natamani hy bahati ya kupendwa ningeipata mm leoo hii nisingekua mama ntiliee labda ningekuaa na kubwa kulizidi manake ningekua na sapoti kubwa zaidi waswahili wanasema kukosea njia ndo kujuaa njia  staki kukuingilia sana kwenye life yako Ila vingine uwege hata unatufikiriaaga na sisi ifikirie na familia yako piaa yes unakosea na still tunakupenda hivyo hivyo”

“Ila ifike wakatii tupee hata barafuu tupoze moyoo manake sio kwa joto hili unalotupaa kiukweli mimi nakuombea kila siku Mungu azidi kukusimamiaa siku mojaa uwe mfano kwa kupitia uloyatenda nyuma nakujua ukiamuaa lako hakuna wa kukuzuia Ila kabla hujafanya kitu kuaa na Wogaa na imani ya wale walokuzunguka”

“Kiukwelii mm nnaposkiaa lolote baya kukuhusuu naumiaa utadhani tunaundugu basii tuu sina lakufanya ila nakuombaa tuonee huruma inatoshaa sasa mamie mengine funika Kombe mwanaharamu apite 🙏🙏🙏”