Joti aiomba Serikali kutenga siku kwa ajili ya kuwaenzi masanii waliokufa na wameacha alama kwa taifa

Msanii mchekeshaji kutoka Tanzania Lucas Mhivule alimaarufu Joti amefunguka mengi kuhusiana na kazi yake lakini pia kuhusiana na sanaa kwa ujumla.
Joti ameogea hayo wakatia anapiga stori na Bongo five siku ya uzinduzi wa tamthilia yake ya Mwantumu ambayo ni msimu wa pili katika ofisi za DStv ambayo itakuwa inaonyeshwa kupitia chaneli namba 160 ya Maisha Magic Bongo kila siku za Jumanne na Jumatano saa moja na nusu usiku.
Mchekeshaji huyo alimtolea mfano marehemu Mzee Majuto na kusema kuwa “Amewafanya vijana wengi kujiingiza kwenye tasnia ya Uchekeshaji na anafaa kuenziwa kwa kutngwa siku maalumu kwa ajili hiyo na sio yeye tu bali wasanii wote ambao walikwisha tangulia mbele ya haki”
Joti ameongea hayo lakini pia akitoa ya moyoni kuhusu zile taarifa zinazosambaa kwamba Watanzania hawaonyeshi ushirikiano na wasanii hadi pale wanapokufa ndio wanaonyesha wanaumuhimu sana na msanii huyo.