Kesi ya Hans Poppe  Kuunguruma Leo Kisutu

Kesi ya Mwenyeketi wa Kamati ya Usajili wa timu ya Simba Zacharia Hans Poppe inatarajiwa kuendelea kusikilizwa leo katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.

Poppe alifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza October 16 na kusomewa mashtaka mawili ambayo ni pamoja na Shtaka la kugushi nyaraka za nyasi bandia kwa ajili ya uwanja wa Simba na kosa lingine ni la kutoa taarifa za uongo kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuhuiana na uhalali wa bei za nyasi bandia za uwanja wa Simba.

Hata hivyo,Hakimu Thomas Simba baada ya makubaliano ya pande mbili kesi hiyo imeunganishwa  na viongozi wengine wa Simba ambao ni Rais  Evans Aveva na Makamu wa Rais Geofrey Nyange “Kaburu”.

Ikumbukwe Mahakama ilitoa amri ya kukamatwa kwa Hans Poppe pamoja na Franklin Lauwo mapema Aprili 30,mwaka huu ili kuweza kuunganishwa katika kesi ambayo inawakabili viongozi hao waliokamatwa juni mwaka jana.

Baada ya wakili wa Takukuru,Leonard Swai kubadilisha hati ya mashtaka na kuwaongeza watuhumiwa hao,baada ya kuwatafuta washtakiwa  hao tangu Machi mwaka huu bila mafanikio hivyo akaomba hati ya kuwakamata washitakiwa hao ambao ,hawakuwepo Mahakamani hapo.

Kwa upande wa Kesi ya inayomkabili aliyewahikuwa Rais wa TFF,Jamal Malinzi na Katibu Selestine  Mwesigwa nayo inatarajiwa kuendelea leo.


Hans Poppe amejisalimisha katika Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) baaada ya kutafutwa kwa muda mrefu ili kuungana na wenzie katika mashataka mawili yanayomkabili ili kesi iweze kusikilizwa katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar.