Ray Atamani Kumpeleka Mtoto Wake Kusoma Majuu

Msanii mkongwe wa filamu za Bongo Movie Vicent Kigosi maarufu kama Ray ameibuka na kukiri kuwa anatamani sana mtoto wake Jaden aende akapate elimu katika nchi za nje.

Ray amefunguka kuwa yupo katika mapambano makubwa ya kufa na kupona ili kuhakikisha mtoto wake wa kipekee Jaden anaenda kupata elimu bora kabisa.

Katika mahojiano yake na Gazeti la Dimba, Ray alisema si kwamba Tanzania hakuna shule bora kwa hapa nyumbani lakini ndoto zake anatamani mwanawe asome nje ya Tanzania kama ambavyo amejiwekea toka awali.

Nilitamani sana mwanangu akasome nje na akikua kidogo tu atasoma moja ya shule bora kabisa, natamani abadilishe mazingira, natambua zipo shule bora sana hapa lakini si mbaya pia akazoee na mazingira mengine, napambana kuhakikisha namwekea akiba ya kutosha ili asipate tabu katika kupata elimu yake”.

Jadrn ni mtoto wa kwanza wa Ray aliyezaa na Msanii mwenzake wa Bongo movie mwanadada Chuchu Hansy.