Msanii wa muziki Bongo, Shilole amesema kuwa hivi karibuni anatarajia kuachia kolabo yake na rapper Chid Benz na nyingine msanii Aslay.

Shilole amesema kolabo hizo ni miongoni mwa nyimbo ambazo ameshazifa ya ukijumlisha na kazi nyingine alizofanya na wasanii wa nje.

“Hivi karibuni nakaribia kutoa wimbo na Chid Benz na ninayo project ambayo nimefanya na project na Aslay hii itakuwa inazungumzia mapenzi,” Shilole ameiambia BongoStarsExclusive.

Kwa sasa Shilole anaendelea kufanya vizuri na wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la Mchaka Mchaka.