Uwoya Adaiwa Kuteketeza Milioni 15 Ndani Ya Siku Moja

Muigizaji wa Bongo movie na mjasiriamali Irene Uwoya adaiwa kutumia shilingi za Kitanzania Milioni 15 kwa siku moja kwa ajili ya Kula bata tu.

Global Publishers wanaripoti kuwa Uwoya alikodi boti kwa mamilioni kisha kuijaza vyakula na vinywaji vya bei mbaya ambavyo navyo viligharimu mamilioni Uwoya alifanya pati hiyo ambayo ilianza muda wa saa 5:00 asubuhi hadi jioni huku akipewa sapoti na baadhi ya wasanii wenzake akiwemo Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ na mama mlezi wa Bongo Muvi, Catherine Ambakisye ‘Mama Loraa’ huku wengine wakipewa mwaliko, lakini hawakuweza kufika.

Kutokana na jeuri ya fedha anayoionesha, Uwoya hivi sasa anadaiwa kutoka na bwana wake mpya ambaye ni raia wa Nigeria. Ilisemekana kwamba jamaa huyo ndiye anayemuwezesha kila kitu Uwoya hivyo Dogo Janja ni wazi kwamba ndiyo  basi tena.

Baada ya taarifa hizo gazeti la Risasi lilimsaka Uwoya ili kumhoji kuhusiana na taarifa hizo ambapo aligunguka:

Niliamua tu kufanya kwa ajili ya mashabiki wangu na timu yangu kwa jumla na ilinigharimu kama zaidi ya shilingi milioni 15 za Kitanzania maana boti yenyewe kuikodisha kwa siku nzima ni kama shilingi milioni tano na hizo nyingine (shilingi milioni 10) zilitumika kwa ajili ya vinywaji na chakula”.

Uwoya alipohojiwa kuhusu kuhusika kwa  tajiri wa Kinigeria alikataa kabisa na kudai ni pesa yake mwenyewe imefanya hayo yote.