Msanii Gigy Money amewatolea uvivu wanaume wasiopenda wake zao kutoka nyumbani na kujishughulisha na kazi nyingine kisa wamezaa.

Gigy Money amesema kuwa mwanamke kuzaa isiwe sababu ya kufungiwa nyumbani muda wote na kuwataka wanaume kubadilika.

“Mimi nisipoenda kazini tutakula nini, acha upumbavu, halafu nyie wanaume badilikieni mwanamke akitaka kutoa ndio umeanza mambo yako , mtu akizaa ndio anakuwa takataka tusizae, tuogope vizazi vetu,” amesema Gigy Money.

Gigy Money ambaye alijipatia umaarufu mkubwa alipokuwa video vixen kwa sasa anafanya vizuri na wimbo Good Time Drip ambao ameshirikishwa na DJ wa Diamond Platnumz, Romy Jones na wasanii wengine kama Producer Abba, Country Boy, Sanja Boy na Queen Darleen.