Msanii wa Bongo Fleva, Nandy ameweka wazi kuwa albamu yake ya kwanza ipo tayari.

Muimbaji huyo amesema kuwa albamu hiyo inayokwenda kwa jina la Single ipo tayari na mashabiki wanaweza kutoa oda za awali na rasmi itatoka November 09, 2018.

“Nina kila sabau ya kumshukuru Mwenyezi Mungu kwani amekua mwaminifu sana kwangu, hatimaye albamu yangu ya kwanza iko tayari kwa Pre-order inapatikana Boom Play Music,” ameeleza Nandy.

Nandy anaingia kwenye orodha ya wasanii waliotoa albamu mwaka huu kama Vanessa Mdee, Wakazi, Diamond Platnumz, Chin Bees na wengineo.  Kwa sasa Nandy anafanya vizuri na wimbo wake mpya uitwao Aibu ambao ameeleza kuwa video yake itatoka hivi karibuni.