Klabu ya soka ya Simba jana Novemba 4 imefanya uchaguzi mkuu wa kuwapata viongozi wapya watakaohudumu kwa miaka minne ijayo kwa mujibu wa Katiba yake.

Uchaguzi huo ulitanguliwa na mkutano wa kawaida wa klabu kwaajili ya kusomewa taarifa mbalimbali za klabu pamoja na kukabidhi madaraka kwa viongozi waliomaliza muda wake wakiongozwa na Kaimu Rais, Dkt Salim Abdallah ‘Try Again’.

Kabla ya kufanyika kwa uchaguzi, wagombea waliruhusiwa kunadi sera zao kwa wanachama jambo lililopelekea kuzuka kwa tafrani pale mmoja wa wagombea wa nafasi ya ujumbe wa bodi, Mwina Seif Kaduguda alipotaka kujua ongezeko la wapiga kura lilivyokuwa.

Zoezi la upigaji kura liliendelea hadi saa 2:00 usiku na kura kuanza kuhesabiwa hadi saa 5:00 usiku ambapo Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Boniface Lihamwike alitangaza matokeo rasmi yaliyompa ushindi mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa klabu, Swedi Mkwabi aliyepata kura za ndiyo 1579 ambazo ni asilimia 79 ya kura zote zilizopigwa.

Katika nafasi za Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi, wagombea waliokuwepo katika uongozi uliopita wameshindwa kutetea nafasi zao ambapo nafasi zote tano zikienda kwa wagombea wapya.

Matokeo ya ujumla katika uchaguzi huo ni haya hapa chini.

Matokeo
Mwenyekiti – Swedi Khamis Mkwabi, kura 1579 kati ya 1628

Wajumbe:
Asha Ramadhan Baraka.    –  1180
Hussein Kitta Mlinga.       –   958
Dr Zawadi Kadunda.         –   830
Seleman Harub Said.     –  740
Mwina Mohamed Kaduguda  –  577
Elia Alfred Martin  –  530
Juma Pinto.            –   440
Jasmin Soud.         –   368
Patrick Rweyemamu –  349
Abubakar Zebo.      –  301
Iddi Kajuna.             –  270
Said Tully.                –   247
Ally Suru.                 –  217
Chris Mwansasu    –  186
Hamis Mkoma.      –  174
Mohamed Wandwi –  124
Abdallah Migomba –  97

Washindi:
1. Hussein Kitta Mlinga
2. Dr. Zawadi Ally Kadunda
3. Seleman Haroub Said
4. Mwina Mohamed Kaduguda
5. Asha Ramadhan Baraka