Yanga Yamtangaza Kaimu Mwenyekiti Wake Mpya

Kamati ya utendaji ya klabu ya Yanga imemteua Thobias Lingalangala kuwa Kaimu Mwenyekiti wa klabu hadi uchaguzi wa kujaza nafasi utakapofanyika January 13 2019

Lingalangala amesema uchaguzi utafanyika kama ulivyotangazwa na kamati ya uchaguzi ya TFF na fomu zimeanza kutolewa rasmi leo ofisi za TFF na klabuni.

Gharama za fomu nafasi ya Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti ni laki 2 na wajumbe ni laki 1.