Leo  ni siku ya kuzaliwa Msanii wa Muziki Nandy (African Princess ) ambapo kama siku yake ya kuzaliwa ameamua kujizawadia gari aina ya BMW.

Ili kuifanya siku hii kuwa  special ameamua kuachia rasmi Album yake ya “The African Princess”.

Msanii huyo kupitia ukurasa wa instagram ametuonyesha zawadi ya gari hilo alilojizawadia na kuandika ujumbe huu.

“HAPPY BIRTHDAY TO ME!!! Naamini kwenye kazi na jasho langu!! baada ya kazi ngumu za hapa na pale si mbaya kujizawadia kidogo ulicho nacho ila shukrani zangu za dhati kwa managment yangu, team yangu, ma fans wangu na wote walioko nyuma yangu,” ameandika Nandy.

“Media zote blogs zote, THT family.. Ni furaha kubwa sana leo kutimiza ndoto ya kuwa na Album yangu i cant wait usiku wa leo pale nextdoor arena, ”ameongeza.