Mali za mfanyabiashara maarufu nchini Yusuf Manji ziko hatarini kufilisiwa na kuwekwa chini ya wadhibiti na wakabidhi wasii ili kulipa madeni yanayodaiwa na Benki ya Maendeleo Afrika mashariki na Kusini, mali hizo ni pamoja na jengo linalofahamika kama Quality Centre.

Taarifa ya wafilisi na wakabidhi wasii chini ya Kampuni ya Price Water House Coopers (PWC) inaeleza kuanzia (jana) Manji hataruhusiwa kumiliki mali hizo mpaka atakapolipa madeni yote.