Katika kuhakikisha kasi ya ujenzi wa miradi ya maji inafanyika kwa kasi kubwa ili wananchi wafaidike na juhudi za serikali.

Halmashauri nchini zimetakiwa kuharakisha malipo ya wakandarasi pindi zinapopelekwa fedha kwenye halmashauri hizo.

Agizo hilo limetolewa leo naibu waziri wa maji,Jumaa Aweso  katika vijiji vya Mtua na. Chimbendenga,wilaya ya Nachingwea mkoa wa Lindi,alipotembelea miradi ya maji inayotekelezwa katika vijiji hivyo.

Uweso alisema  baadhi ya halmashauri zimekuwa zikichelewesha malipo ya wakandarasi hata baada ya wizara kutuma fedha kwa ajili ya malipo.Hali ambayo inasababisha kazi ya ujenzi ya miundombinu kusuasua.Kutokana na wakandarasi kutolipwa.

Alisema wizara hiyo haipendi kuwa kikwazo cha upatikanaji maji kwa wananchi kupitia miradi mbalimbali inayotekelezwa nchini.Kwahiyo halmashauri zinawajibu wa kuharakisha mchakato wa malipo kwa wakandarasi mara tu zinapotumiwa fedha.

Alisema kuwalipa wakandarasi kwa wakati kutasababisha ujenzi wa miradi hiyo kuharakishwa.Hali itakayosababisha miradi ikamikike kwa wakati.Hivyo wananchi wataondikana na tatizo la maji katika maeneo yao.Kwani hiyo ndiyo nia ya serikali.

“Wizara hii siyo ya ukame,bali ya maji.Inawajibu wa kuhakikisha wanachi wanapata maji safi na salama.Nasio maji tu bali safi na salama,”alisisitiza Uweso.

Aidha naibu waziri huyo aliwataka wakuu wa idara na mamlaka za maji kutosita kuwachukulia hatua wakandarasi wababaishaji wanaochelewa kumaliza kazi na wanaolipwa fedha nakwenda kufanyia kazi nyingine tofauti na niradi husika.

Abainisha kwamba miongoni mwachangamoto zilizopo ni kuwepo wakandarasi wababaisha ambao kwa miaka mingi waliifanya wizara hiyo kama sehemu ya kupatia fedha kwa ajili ya kununulia magari na kujengea majumba ya kifahari.

Katika kulipa nguvu agizo lake,Uweso aliwataka maofisa hao kuwa makini wakati wa zoezi la uteuzi wa wakandarasi.Kwakuziteuwa kampuni zenye uwezo.Ikiwemo vifaa vya kazi na mitaji ya kutosha kufanyia kazi.Huku wakepuka upendeleo katika utelezaji wa zoezi la uteuzi wakandarasi.

“Msiwateuwe wakandarasi kwa vigezo vya ushemeji au ujomba,zingatieni sifa na vigezo.Wahandasi! msiwabembeleze wakandarasi,wanaoshindwa waondoeni kwani tunataka miradi ikamilike kwa wakati,”aliongeza kusema Uweso.

Mbali ya kutoa maagizo hayo kwa halmashauri,wakuu wa idara na maofisa wa idara za maji.Naibu waziri Uweso aliwaonya wakandarasi wenye tabia ya kubadilisha matumizi ya fedha wanazolipwa.Akiweka wazi kwamba serikali haitawavumilia.

Alisema miongoni mwa sababu za kuchelewa kukamilika kwa baadha ya miradi nitabia ya baadhi ya wakandarasi kupeleka kwenye kazi za miradi mingine badala ya kazi husika.Tabia ambayo hainabudi kukoma.