Wanajeshi wawili waliokolewa. Mmoja wao yuko hali nzuri kwa mujibu wa wa wizara ya ulinzi nchini Japan. Hali ya mwanajeshi mwingine haikujilikana mara moja.

Ndege hizo zilikuwa za KC-130 na F/A-18 kutoka kambi ya Iwakuni karibu na Hiroshima.

Vyombo vya habari vya Marekani vinasema ndege hizo zilianguka wakati wa kuongezwa mafuta zikiwa angani.

Jeshi la wanamaji halijathibitisha rasmi hilo likitaja kisa hicho kuw hitilafu.

Kulikuwa na wanajeshi watano kwenye ndege ya C-130 na wawili kwenye ndege ya F-18. Mmoja wa wale waliookolewa alikuwa kwenye ndege ya kijeshi, kwa mujibu wa maafisa wa Japan.

Taarifa kwennye mtandao wa Facebook iliyochapiswa na kikosi cha wanamaji ilisema ajali hiyo ilitokea umbali wa kilomita 320 ktoka pwani.

Ndege za Marekani zilikuwa zimepaa kutoka kambi ya Iwakuni na zilikuwa kwenye mazoezi ya kawaida wakati hitilafu hiyo ilitokea.

Waziri wa ulinzi nchini Japan Takeshi Iwaya alisema ndeege tisa za Japan na meli tatua zinashiriki katika oparesehni ya uokoaji.