Msanii wa filamu nchini Rammy Galis ametoa ahadi ya kumuingiza mtoto wa aliyewahi kuwa mpenzi wake marehemu Agness Masogange, Samira katika soko la filamu kama alivyiofanya kwa mama yake.

Rammy amefunguka hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusiana na uzinduzi wa filamu yake mpya aliyocheza na marehemu Agness Masogange, amesema kuwa amemshirikisha mtoto huyo kufatia kipaji kikubwa alichokiona ndani yake.

” nina mpango wa kumuingiza katika soko la filamu kwasababu mtoto wa Agness anakipaji kikubwa sana cha kuigiza na nitakua nae mwanzo hadi mwisho maana hata baba yake amekubaliana na suala hilo la mwanae kuingia kwenye sanaa” amesema Rammy.

 Amesema filamu hiyo inayotarajiwa kuzinduliwa Desemba 15, mwaka huu katika ukumbi wa Citymall jijini Dar es Salaam itakwenda kwa jina la Hukumu,ambapo amefunguka kuwa aliamua kumshirikisha Masogange lengo likiwa ni kuhakikisha anamuhamishia katika upande wa uigizaji moja kwa moja.

Aidha ametoa shukrani za dhati kwa mashabiki wote wanaosimama na kuziunga mkono kazi zote anazozifanya, pia ametoa rai kwa mashabiki kujitokeza kwa wingi siku ya uzinduzi wa filamu hiyo.

 “niliamua kumshirikisha Masogange kwenye filamu hii ya hukumu lengo langu likiwa ni kumuona anafanya kazi zake katika mpangilio nilimuona ameanza kupotea katika upande wa video queen hivyo nikaamua nimuhamishie kwenye sanaa ya filamu maana niliamini anaweza na alifanya vizuri.

nawashukuru sana mashabiki zangu niwahimize tu wajitokeze kwa wingi ili tuweze kukamilisha zoezi hili la uzinduzi wa movie yetu ya Hukuma,”amesema Rammy.

Kwa upande wake Samira amesema kuwa anamshukuru Rammy Galis kwa kuhakikisha anasimamamia kuingia kwake katika tasnia ya filamu,pia ametoa shukrani zake baba yake kwa kumuunga mkono.

Samia amefunguka kwa kusema watanzania wake tayari na kumpokea katika soko la filamu.

“Namshukuru sana uncle Rammy kwa kunisaidia vingi tangu marehemu mama yangu kufariki ameniahidi vingi yote hayo ikiwa ni kunisaidia kimaisha hasa katika upande wa sanaa,pia nawashukuru sana wote waliokuwa wakinitia moyo hasa katika kipindi kigumu nilichokuwa napitia ninaahidi kuingia kwenye sanaa ili niendeleze kipaji cha mama yangu,”amesema Samira.

aliongeza kuwa;”nawapenda sana wasanii wa bongo movie nampenda Aunty Ezekiel, Wema Sepetu, Rammy, na Hashim Kambi”.