Imeelezwa kuwa katika nchi za Afrika Mashariki Tanzania inaongoza kwa kivutio cha uwekezaji ambapo imefikia jumla ya uwekezaji 1458.

Hayo yamebainishwa Leo Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha uwekezaji Tanzania TIC Godfrey Mwambe katika mkutano wa waandishi wahabari.

Mwambe amesema TIC ikiwa katika kuhamasisha, kushawishi na kuratibu uwekezaji nchini, imefanikiwa kuwekeza takribani billion 1.3 ambapo ambapo nchini Uganda imefikia million 570.

Amesema katika kipindi cha miaka mitatu nchi nyingi Duniani uwekezaji ulishuka lakini Tanzania imekuwa na kivutio kikubwa cha mazingira wezeshi ya uwekezaji ambapo imepata miradi 905.

Pia amesema kuna miradi mbalimbli ambayo serikali imeteleza kuwekeza ndani na nje ya nchi.

Hata hivyo amesema Tanzania imejikita hasa katika kujenga urafiki na Jamhuri ya China, ili kuwavutia kuwekeza kujenga viwanda mbalimbali ili kuwezesha Tanzania kufikia uchumi wa kati, kwa mujibu wa Sera ya Serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Tanzania ya viwanda.