Mzazi mwenza wa staa wa Bongo fleva nchini Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’, Fahyma au Fahyvanny amedai kuwa yeye na baba watoto wake wamefunga ndoa ya Siri.

Fahyma ameweka wazi kuwa yeye na mzazi mwenzie wameshafunga ndoa kwa siri kilichobaki kati yao ni sherehe tu na kufanya watu wengi kupata na maswali.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa, Fahyma alisema alichokiandika katika mtandao wake kuhusu ndoa yake na mzazi mwenziye huyo ni kweli na siku za hivi karibuni ataweka wazi kuhusu taratibu za sherehe yao.

Nilichokiandika nilikimaanisha kuwa ndoa tumeshafunga kama ambavyo imeonekana kwenye mitandao na kilichobaki ni kufanya sherehe tu ambayo tutatangaza hivi karibuni taratibu zote kwa sababu bado kuna mambo hayajakaa sawa ndio maana hatujaweka wazi kuhusu ndoa tuliyofunga ni ya dini gani na tulifungia wapi yote mtafahamu, lakini kwa sasa siwezi kuzungumza chochote zaidi ya hayo“.

Rayvanny na Fahyma walikutana kutokana na kazi zao ambapo Rayvanny ni Msanii na Fahyma kuwa video vixen na Baada ya kuwa pamoja kwa muda mrefu wamefanikiwa kuzaa Mtoto mmoja anayeitwa Jayden.