Mwanamuziki wa muziki wa Bongo fleva Harmonize na Mpenzi Wake Sarah wamezima tetesi zilizokuwa zinasambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa wameachana.

Harmonize na Sarah wameachia kipande cha Video kinachowaonyesha wakiwa wanacheza wimbo mpya wa Harmonize aliomshirikisha Rayvanny ‘Para nawe’ na kukumbatiana kimahaba na kuonyesha kuwa wapo pamoja.

Kipande hicho cha video kimewekwa mtandaoni na Harmonize mwenyewe pamoja na mpenzi wake huyo ikiwa ni siku chache baada ya kuripotiwa kuwa wamemwagana kisha kurudi kwa mpenzi wake wa zamani, Jackline Wolper.

Tetesi za kuvunjika zilianza Baada ya Harmonize kuanza kuonekana pamoja na Harmonize katika tamasha la Wasafi Festival na hata kukumbatiana stejini huku Mpenzi Wake Sarah akiwa nje ya nchi na kupelekea tetesi za kuachana.