Mbwa aliyekuwa amepewa kazi ya kuwa msaidizi wa Rais wa 41 wa Marekani George HW Bush amepigwa picha akionekana kuomboleza karibu na jeneza la kiongozi huyo.

Bush, aaliingia madarakani mwaka 1989 hadi 1993 alifariki dunia Ijumaa iliyopita usiku akiwa na miaka

Sully, mbwa wa jamii ya golden labrador, alisafiri pamoja na mwili wa marehemu kwenye ndege kutoka Texas kwenda Washington DC siku ya Jumatatu.

Jeneza lenye mwili wake lilisafirishwa kwa ndege kutoka Texas kwenda DC kwa ndege ya Air Force One – ambayo kwa muda ilipewa jina Special Air Mission 41, kwa heshima ya rais huyo. Mwili huo ulirejeshwa Texas Jumatano.

Picha ya kwanza kabisa juu ya Sully akitoa heshima zake ilipakiwa mtandaoni na msemaji wa Bw Bush Jim McGrath, pamoja na ujumbe: “Mission complete”

Sully amepewa jina la rubani wa ndege za abiria Chesley “Sully” Sullenberger, ambaye alifanikiwa kuielekeza ndege ya kubeba abiria kutua kwa dharura kwenye Mto Hudson mwaka 2009, na kuwaokoa abiria wote 155 na wahudumu waliokuwa kwenye ndege hiyo.

Mbwa huyo mwenye miaka miwili alikabidhiwa jukumu la kuwa mbwa msaidizi wa Bush aliyekuwa akitumia kiti cha magurudumu mapema mwaka huu.

Watu katika mitandao ya kijamii wamekuwa wakimshukuru Sully kwa huduma zake, na kwa kawaida kuzungumzia uaminifu wa mbwa kwa wamiliki wao. Watu katika mitandao ya kijamii wamekuwa wakimshukuru Sully kwa huduma zake, na kwa kawaida kuzungumzia uaminifu wa mbwa kwa wamiliki wao.