Msanii wa filamu nchini ambaye pia ni mwanamitindo, Jackline Wolper amefunguka juu ya mpango wa kujizawadia katika kumbukizi yake ya siku yake ya kuzaliwa.

Akizungumzia juu ya zawadi hiyo, Wolper amesema kuwa amejizawadia kukua na kuacha mambo ambayo yalikuwa yanakwamisha maendeleo yake kwenye maisha.

Kama ilivyo ada ya kujipa zawadi katika ‘birthday’ zangu, hii ya sasa nimekua na kubadilika na hii ndio zawadi niliyoamua kujipa, nimekuwa ‘very strong’ japokuwa napitia vikwazo vingi katika kazi zangu na maisha kwa ujumla lakini napambana“, amesema Wolper.

Wolper pia amezungumzia mahusiano yake, ambapo amesema kuwa amejifunza kuwa na mahusiano na mtu ambaye anamzidi akili, pesa na elimu na kusema kuwa kwa sasa amekuwa kwenye mahusiano na mtu wa aina hiyo.

Ukiwa mswahili na huna kiwango kikubwa cha elimu, basi inabidi utafute mtu ambaye amekuzidi ili akusaidie kubadili maisha yako, nina mwaka sasa nina ‘date’ na mtu ambaye amenitoa kwenye uswahili na kunirudisha kwenye uzungu, nimebadilika sasa hivi naweza kushirikiana na eX’ wangu kwenye mambo muhimu tofauti na zamani, nimefundishwa kuondoa kinyongo moyoni“, ameongeza.