Wasanii wa muziki wa kizazi kipya Dogo Janja pamoja na Diamond Platnumz wamekuwa miongoni mwa wasanii wanao toa msaada kwa vijana wengi wenye matatizo. Hii imetokea baada ya wasanii hao kutoa msaada kwa kijana anayeitwa Rajabu mwenye matatizo ya Kansa ya mifupia.

Kijana huyo amepata msaada kwa Wasanii hao akiwa anatakiwa kwenda kutibiwa nchini India, na Dogo Janja ametoa msaada wa shilingi za Kitanzania milioni mmoja.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Dogo Janja ameandika kuwa

” Niliposema nimeumizwa na kijana mwenzangu Rajabu nilimaanisha,nimekabidhi shilingi milioni moja kwa wahusika wanaomuhudumia,sitoi kwa kuwa zimezidi”